19 Machi 2011 - 20:30

Nchini Misri waandamanaji wawili wameuawa baada ya kufyatuliwa risasi katika mji wa Alexandria. Katika mji mkuu Cairo mtu moja ameauwa na wengine 600 kujeruhiwa baada ya polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji katika Medani ya Tahrir.

Ripoti ya ABNA-Maandamano hayo ya Cairo na Alexandria yaliitishwa na wananchi wanaolipinga baraza la kijeshi linalotawala nchini humo. Wamisri wanataka watawala wa kijeshi wakabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia. Waandamanaji wanasema utawala wa kijeshi unaaongozwa na Field Marshal Hussein Tantawi hauna azma ya kutekeleza mabadiliko na kuwafuta kazi vibaraka wa utawala ulioangushwa wa dikteta Mubarak. Watawala wa kijeshi Misri wanasema uchaguzi wa rais utafanyika mwakani.